Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mnyama kamili gado kuwavaa Wachimba Dhahabu

Kibu Simba SC .jpeg Mnyama tayari kuwavaa Wachimba dhahabu

Mon, 12 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Leo saa 10 jioni kikosi cha Simba kitashuka katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza kuikabili Geita Gold katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC.

Simba wataingia katika mchezo wa leo wakiwa na kumbukumbu ya kupata sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Azam FC ambao ulifanyika kwenye Uwanja wa CCM Kirumba siku ya Ijumaa.

Simba inafahamu utakuwa mchezo mgumu lakini lengo lao ni kupambana kupata pointi tatu muhimu.

Benchi la Ufundi latoa mikakati ya mechi ambapo Kocha wa Makipa, Daniel Cadena amesema maandalizi ya mchezo yamekamilika na wachezaji wapo kwenye hali nzuri.

Cadena amesema pamoja na ugumu wa ratiba kuwa ngumu watacheza kila baada ya siku mbili lakini wamejipanga kuhakikisha wanashinda.

Cadena amesema malengo ni kushinda kila mchezo uliopo mbele yao kwa kuwa wanahitaji kutwaa ubingwa wa Ligi msimu huu.

“Tupo tayari kwa mchezo wa leo, haitakuwa mechi rahisi kutokana na ubora wa wapinzani na jambo jema ni kwamba hatuna mchezaji majeruhi,” amesema Cadena.

Mlinzi wa kati Hussein Kazi amesema malengo yao ni kuchukua taji hivyo wanahitaji kushinda kila mchezo ni kama fainali.

Kazi amesema Geita ni timu nzuri na haijawahi kuwa mechi nyepesi kucheza dhidi yao lakini kila mchezaji anajua umuhimu wa kupambana hadi mwisho kufanikisha malengo.

“Ligi ni ngumu, kwetu kila mchezo ni fainali. Bado tupo kwenye kupigania ubingwa mechi bado ziko nyingi na tunaanza kesho dhidi ya Geita,” amesema Kazi.

Aidha, wachezaji wote wapo kwenye hali nzuri na hakuna yoyote ambaye amepata maumivu ambayo yatamfanya kuukosa mchezo wa leo.

Wachezaji hao jana jioni wamefanya mazoezi ya mwisho katika Uwanja wa CCM Kirumba na wapo tayari kwa mchezo wa leo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live