Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mnyama alivyofufukia Kizimkazi

Fuul Time Simba Simba SC

Thu, 25 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya ukame wa michezo mitano pasi na ushindi, mnyama Simba SC jana, Aprili 24, 2024 alifufuka kwa kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya KVZ, katika michuano maalumu ya Kombe la Muungano ikiwa sehemu ya Maadhimisho ya Miaka 60 ya Muungano.

Kabla ya ushindi wa jana, ushindi wa mwisho wa Simba ulikuwa Machi 15, dhidi ya Mashujaa FC kwenye mchezo wa Ligi, lakini baada ya hapo walipoteza michezo miwili dhidi ya Al Ahly (CAFCL), wakapoteza kwa penati mchezo dhidi ya Mashujaa (CRDB), sare dhidi ya Ihefu (Ligi Kuu), kipigo dhidi ya Yanga (Ligi Kuu).

Dakika 25' zimetosha kwa Freddy Koublan kuwainua vitini mashabiki wa mnyama Simba katika Uwanja wa New Amaan complex, visiwani Unguja, Zanzibar.

Dakika 90'+4 Israel Mwenda anaihakikishia Simba kutinga hatua ya fainali ya michuano hiyo ikiwa ni marejeo ya baada ya kufanyika miaka 20 iliyopita.

Nusu fainali ya pili itachezwa leo, Azam FC watakapokabiliana na KMKM majira ya saa 2:15 usiku.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live