Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mnunka: Nilifikiria kufunga mabao 25

Mnunka C.jpeg Aisha Mnunka

Mon, 27 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati Simba Queens wanahitaji pointi moja ili kujihakikisha ubingwa wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania msimu huu, kinara wa kupachika mabao, mshambuliaji wa timu hiyo, Aisha Mnunka, amesema malengo yake makuu ni kuona wanatwaa taji la msimu huu.

Mnuka na Stumai Abdallah wa JKT Queens, wote wakiwa Watanzania wanachuana vikali kuwania kiatu cha dhahabu.

Straika huyo wa Simba Queens akiwa ametikisa nyavu mara 18 wakati Stumai amefunga magoli 16.

"Nikipata nafasi natumia kwa sababu nataka timu yangu ishinde, lakini lengo langu la pili ni kuwa mfungaji bora, mwanzoni malengo yangu yalikuwa kufunga mabao 25, naona natakiwa kuzidisha ili kuwa mfungaji bora," alisema Mnunka.

Katika msimamo wa ligi hiyo itakayorejea tena dimbani kuanzia Juni 7, mwaka, Simba Queens inaongoza ikiwa na pointi 43 na JKT Queens, mabingwa watetezi wakiwa nafasi ya pili na pointi 34 kibindoni.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live