Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mnigeria aionya Yanga

John Noble Kipa wa Tabora United Mnigeria, John Noble

Thu, 21 Dec 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Kipa wa Tabora United Mnigeria, John Noble amesema huu ni muda wa kuonyesha ubora unaozungumzwa na mashabiki wakati timu hiyo itakapokuwa na kibarua kigumu dhidi ya Yanga Jumamosi kwenye Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.

Akizungumza na Mwanaspoti, kipa huyo aliyejiunga na timu hiyo msimu huu akitokea Enyimba amesema kama wachezaji ni wazi wanatambua ugumu uliopo ila wamejipanga ipasavyo kukabiliana na wapinzani wao kwa lengo la kupata pointi tatu.

“Kila mchezo ni mgumu kama iliyopita na sisi wachezaji jukumu letu ni kuhakikisha tunapambana kwa ajili ya timu, hii ni nafasi nyingine ya kuonyesha ukubwa tuliokuwa nao kwa sababu uwezo na uzoefu tunao wa kukabiliana na yoyote,” alisema.

Noble ameongeza licha ya kutoka kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi ambao hutumia kwa michezo ya nyumbani na kuhamishiwa Jamhuri ila haitowaathiri kwa kiasi kikubwa kutokana na ukaribu wa miji hiyo japo wanawakosa mashabiki wao halisia.

“Yanga ina wachezaji wazuri na siwezi kusema mmoja wao aliyekuwa hatari kwa sababu naona wanacheza kitimu zaidi na kila mtu ana morali anapopata nafasi ya kucheza hivyo itakuwa mechi ngumu lakini tutapambana kadri ya uwezo wetu kushinda.”

Mchezo huu utakuwa ni wa kwanza wa Ligi Kuu Bara kwa timu hizi kukutana tangu Tabora United ilipopanda rasmi msimu huu ambapo katika michezo 12 iliyocheza imeshinda mitatu, sare sita na kupoteza mitatu ikishika nafasi ya 10 na pointi 15. Mara baada ya mechi hiyo, Tabora United itajiandaa kwa mchezo mwingine dhidi ya Simba uliopangwea kupigwa Desemba 29, japo kuna hatihati ya kuchezwa kulingana na uwepo wa michuano ya Kombe la Mapinduzi 20245 itakayoanza rasmi Desemba 28 visiwani Zanzibar.

Mechi ijayo

Des 22, 2023

Tabora Utd v Yanga (Saa 10:00 jioni)

Des 29, 2023

Tabora Utd v Simba (Saa 10:00 jioni)

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: