Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mmiliki wa Timu amtimua Kocha kisha yeye kujitangaza kocha

Fabio Celestini Mmiliki wa Timu amtimua Kocha kisha yeye kujitangaza kocha

Tue, 28 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mmiliki na Mwenyekiti wa klabu ya FC Sion ya Uswisi, Christian Constantin (kushoto PICHANI) amemsimamisha kazi kwa muda kocha mkuu wa klabu hiyo, Fabio Celestini (kulia) na kujitangaza kama kocha wa muda kufuatia kipigo cha 4-0 cha klabu hiyo dhidi ya St Gallen siku ya Jumamosi kwenye mchezo wa Ligi kuu Nchini humo.

Ripoti zinadai Mmiliki huyo mwenye umri wa miaka 66 ataiongoza klabu hiyo kwenye michezo miwili ijayo ya klabu hiyo dhidi ya FC Lugano.

Taarifa ya klabu hiyo kwa Umma imesema:- “FC Sion imemsimaisha kwa muda mkufunzi Fabio Celestini kwa kipindi cha Wiki moja.”

"Wakati huo huo Christian Constantin atachukua nafasi yake kuiongoza timu na atakuwa kwenye benchi la FC Sion kwa ajili ya michezo miwili ijayo dhidi ya FC Logano." Imesema taarifa hiyo.

Celestini aliteuliwa kuwa kocha mkuu wa FC Sion mnamo Novemba kuchukua nafasi ya Paolo Tramezzani aliyefutwa kazi lakini ameshinda mechi moja tu kati ya 8 aliyoiongoza klabu hiyo.

FC Sion ipo nafasi ya 9 kwenye msimamo wa Ligi kuu Uswisi ikiwa na alama sawa na wahanga wa kushuka daraja FC Winterthur.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live