Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mmiliki wa Liver alivyotumia pesa ndefu kwenye usajili

Liverpool Vs Villa Mmiliki wa Liver alivyotumia pesa ndefu kwenye usajili

Sat, 11 Nov 2023 Chanzo: Mwanaspoti

John Henry ameiongoza Liverpool kwa mikataba ya pesa ndefu wakati wa utawala wake kama mmiliki mkuu wa klabu hiyo.

Henry na Fenway Sports Group walikamilisha ununuzi Liverpool kwa Pauni 300 milioni Anfield Oktoba mwaka 2010, wakichukua nafasi ya Wamarekani wawili Tom Hicks na George Gillett. Tangu wakati huo, Liverpool imeshinda karibu kila taji kubwa katika kipindi cha miaka 13 iliyopita.

FSG ilimwajiri Kocha Jurgen Klopp Oktoba mwaka 2015 na wameshinda mataji saba makubwa. Sehemu ya mafanikio hayo yametokana na biashara ya uhamisho wa wachezaji ambayo klabu imefanya katika miaka ya hivi karibuni.

Dirisha la uhamisho wa majira ya kiangazi la 2023 tumeshuhudia wachezaji wanne waliosajiliwa wakiwasili Merseyside - Dominik Szoboszlai, Alexis Mac Allister, Wataru Endo, na Ryan Gravenberch. Katika miaka 13 ambayo Henry na FSG wamemiliki Liverpool, wamemwaga pesa nyingi kwa ajili ya uhamisho wa wachezaji. Hawa hapa mastaa 10 waliosajiliwa chini ya mmiliki huyo kwa kutumia mkwanja mrefu.

10) Fabinho - Pauni 43.7 milioni

Liverpool ilimilisha uhamisho wa Fabinho kutoka Monaco mwaka 2018,saa chache baada ya kupoteza fainali ya Ligi Mabingwa Ulaya dhidi ya Real Madrid. Kiungo huyo akiwa na uzi wa Liverpool ameshinda mataji manne makubwa msimu wa 2019-2020. Katika usajili wa kiangazi Fabinho alijiunga na Al-Ittihad kwa Pauni 40 milioni.

9) Mohamed Salah - Pauni 43.9 milioni

Ilikuwa kwenye usajili dirisha la kiangazi mwaka 2017 Liverpool ilipomsajili Salah kutoka Roma, fowadi huyo akashinda ndoo ya Ligi Kuu England kwa mara ya kwanza tangu alipoondoka Chelsea. Salah amekuwa mchezaji muhimu Anfield kutoka na mchango wake na aliweka rekodi ya kuwa mfungaji bora wa muda wote Liverpool. Salah anahitaji zaidi ya mabao manne afikishe mabao 200 katika mashindano yote.

8) Cody Gakpo - Pauni 44 milioni

Liverpool ilimsajili Cody Gakpo kutoka PSV Eindhoven katika dirisha dogo la usajili la kiangazi mwaka huu. Gakpo alihusishwa na Manchester United lakini akachagua Liverpool. Bao la kwanza kufunga ilikuwa dhidi ya Man United katika ushindi wa mabao 7-0 uwanja wa Anfield.

7) Diogo Jota - Pauni 45 milioni

Straika huyo wa kimataifa wa Ureno alijiunga na Liverpool kutoka Wolves mwaka 2020, akifuatiwa na Thiago Alcantara ambaye alisajiliwa. Mreno huyo alifunga mabao 47 kwenye mechi 126 tangu alipotua Anfield. Baada ya Roberto Firmino kuondoka, umuhimu wa Jota ukaanza kuonekana kwa kasi na amejumuishwa kwenye kikosi cha kwanza mara kwa mara.

6) Luis Diaz - Pauni 50 milioni

Ilikuwa mwaka jana Liverpool ilipoamua kumsajili Luis Diaz kutoka Porto, wiki mbili tu baada ya timu hizo kumenyana kwenye Ligi Mabingwa Ulaya. Diaz alisajiliwa kwa ajili ya kuziba pengo la Sadio Mane ingawa aliumia Oktoba mwaka jana na akawa nje ya dimba msimu mzima wa 2022-2023, lakini baada ya kurejea akiwa fiti amekuwa mchezaji tegemeo.

5) Naby Keita - Pauni 52.75 milioni

Kiungo huyo alisajiliwa kwa mkwanja mrefu chini Klopp akiwasili akitokea RB Leipzig mwaka 2018 baada ya kukubali mkataba wa miezi 12. Keita alikuwa sehemu ya kikosi kilichobeba mataji makubwa msimu wa 2019-2020. Hata hivyo, majeraha yalichangia kiwango chake kushuka na kutemwa kikisoni. Kwa sasa anakipiga Werder Bremen.

4) Dominik Szoboszlai - Pauni 60 milioni

Moja kati ya usajili mpya wa Liverpool, Dominik Szoboszlai aliwasili akitokea RB Leipzig dirisha la kiangazi lililopita. Tayari ameshajitengenezea umaarufu tangu alipotua, amecheza mechi zote dakika 90 za Ligi Kuu England.

3) Alisson Becker - Pauni 65 milioni

Liverpool ilimsajili kipa huyo mwaka 2018 kwa mkwanja mrefu uliovunja rekodi ya usajili. Usajili huo ulivunja rekoidi ya usajili wa kipa wa Chelsea Kepa Arrizabalaga. Msimu wa kwanza Allison aliiongoza Liverpool kubeba ubingwa wa Ligi Mabingwa Ulaya ikifuatiwa na ndoo ya Ligi Kuu England.

2) Virgil van Dijk - Pauni 75 milioni

Beki huyo wa kimataifa wa Uholanzi Januari mwaka 2018 akitokea Southampton. Ni beki mwenye uzoefu na imara katika safu ya ulinzi ya Liverpool. Van Dijk ni nahodha wa timu baada ya Jordan Henderson kutimkia Saudi Arabia.

1) Darwin Nunez - Pauni 85 milioni

Alitua mwaka jana Benfica, straika huyo alionyesha kiwango bora kwenye mechi ya Ligi Mabingwa Ulaya dhidi ya Liverpool kabla ya kusajiliwa. Licha kupitia kipindi kugumu.

Chanzo: Mwanaspoti