Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mmesikia? Kisa cha Onana kufungwa fungwa mabao hiki

Andre Onana Miss 7 Mmesikia? Kisa cha Onana kufungwa fungwa mabao hiki

Sun, 8 Oct 2023 Chanzo: Mwanaspoti

WASOMA mchezo wa timu pinzani wameripotiwa kuwaambia wachezaji wao kutumia udhaifu wa kipa Andre Onana wakati wanapokabiliana na Manchester United ili kuwaadhibu.

Onana, 27, ambaye ni kipa Mcameroon, alijiunga na chama hilo la Erik ten Hag akitokea Inter Milan kwa ada ya Pauni 47.2 milioni, amekosolewa kwelikweli kwa wiki za hivi karibuni kutokana na kufanya makosa makubwa yanayoigharimu timu yake.

Kwa wastani, Onana ameruhusu karibu mabao mawili katika kila mechi aliyochezea Man United. Usiku wa Jumanne iliyopita aliigharimu Man United pakubwa kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Galatasaray na kupoteza mchezo huo wakiwa nyumbani Old Trafford.

Kwa namna alivyojipanga kwenye bao la Mauro Icardi ni kitu kilichoibua maswali mengi, huku pasi yake mbovu iliyotua kwenye miguu ya Dries Mertens ndiyo iliyomsababishia Casemiro aonyeshwe kadi nyekundu baada ya Mbrazili huyo kulazimika kwenda kufanya rafu ndani ya boksi akijaribu kuokoa mambo.

Icardi alikosa mkwaju wa penalti hiyo, lakini tayari kila kitu kilitibuka. Kipa Onana sasa ameruhusu mabao saba kwenye mechi mbili za Ligi ya Mabingwa Ulaya – rekodi ambayo timu pinzani zinaweza kutazama na kuona ni udhaifu wanaoweza kuutumia.

Ripoti zinadai kwamba timu pinzani sasa zimeanza kumfuatilia Onana namna anavyojipanga kuona kama wanaweza kutumia fursa za kumfunga, huku jambo hilo likifanywa na wachambuzi wa mchezo wa timu pinzani. Kipa huyo ambaye kiwango chake kwa sasa kimekuwa hovyo sana, mara nyingi amekuwa akijipanga kwenye eneo ambalo linawapa wapinzani wepesi wa kufunga.

Onana inadaiwa kwamba anakuwa kwenye eneo lenye hatari ya kufungwa wakati Man United inapokuwa haina mpira. Na kinachoelezwa ni kwamba wasoma mchezo wa timu pinzani sasa wamewaagiza wachezaji wao kuhakikisha wanatumia fursa hiyo kwa sababu wanakuwa kwenye nafasi kubwa ya kufunga bao.

Kocha Ten Hag amemsajili Onana kutokana na sababu nyingi tofauti, ikiwamo ya uwezo wake wa kucheza mpira kuanzia nyuma. Lakini, pasi zake za hovyo zimeifanya Man United kwenye kwenye mashaka makubwa na kuruhusu mabao.

Kocha Ten Hag bado anamsapoti kipa wake kwamba atakuja kuwa mmoja wa makipa bora kabisa duniani baada ya mechi ya Galatasaray licha ya kuboronga.

Kitu ambacho kinashangaza, kipa ambaye alionekana hajui, David De Gea amekuwa makini zaidi mpira unapokuwa kwenye miguu yake, licha ya kwamba ana wastani wa asimilia 68.33 wa usahihi wa pasi zake ukilinganisha na Onana mwenye wastani wa asilimia 74.14.

De Gea amekuwa na wastani mzuri wa kuokoa, asilimia 70%, wakati Onana amekuwa na wastani wa asilimia 66.67, huku mashabiki wakipata shaka kwamba kipa huyo shuti likilenga golini tu ni bao.

Hata hivyo, inaelezwa kwamba Onana kwa sasa amekumbana na wastani wa mashuti sita kwa dakika 90, wakati De Gea alikuwa na wastani wa mashuti matatu kwa mechi, jambo linalofichua kwamba safu ya mabeki ya miamba hiyo ya Old Trafford kwa sasa ina matatizo makubwa.

Mwisho wa msimu kutapatikana takwimu nzuri za kulinganisha, lakini kipa huyo mpya wa United, ambaye ni chaguo la kwanza kwa sasa, Onana bado ana safari ndefu.

Chanzo: Mwanaspoti