Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mmarekani wa Yanga ‘deal done’ hadi 2025

Mzungu Yanga Mmarekani wa Yanga ‘deal done’ hadi 2025

Thu, 4 Jan 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Baada ya kufanya mazoezi na Yanga Princess kwa miezi mitatu, Kaeda Wilson raia wa Marekani amesaini mkataba wa mwaka mmoja kuwatumikia wananchi hao.

Mchezaji huyo anayecheza nafasi ya kiungo awali alikuja na wazazi wake likizo nchini na kudai kama Yanga itaridhia kuwa naye basi kwao hawana shida.

Akizungumza na Mwanaspoti jana, baba mzazi wa kiungo huyo Reggie Wilson alithibitisha mwanaye amesaini mkataba huo, huku akitaja sababu ya kutoonekana uwanjani ni kuchelewa kupata kibali cha kazi. Alisema Shirikisho la Soka Marekani ndilo limechelewesha kutoa kibali cha uhamisho kutokana na Sikukuu za Krismasi na Mwaka Mpya siku ambazo wafanyakazi hawaingii ofisini.

“Natumai leo tutapewa kibali cha uhamisho, kinachosubiriwa ni namba tu lakini ni kweli amesaini mkataba na vitu vikikaa sawa mtamwona uwanjani,” alisema baba mzazi wa mchezaji huyo aliyekuwa kwenye akademi ya 7 Elite ya Marekani.

Yanga dirisha hili dogo tayari imesajili straika kutoka Kenya, Janet Bundi na katika mchezo wake wa kwanza alitupia mabao mawili kwenye ushindi wa 6-1 dhidi ya Amani Queens, Ligi Kuu ya wanawake Bara Desemba 27.

Chanzo: Mwanaspoti