Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mmachinga: ‘Yes’ Kagere mashine

KAGERE Mmachinga: ‘Yes’ Kagere mashine

Fri, 29 May 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

BAADA ya kuitazama kasi ya mshambuliaji wa Simba, Meddie Kagere katika kupachika mabao, straika nyota wa zamani wa Yanga, Mohammed Hussein 'Mmachinga' amesema ana imani Mnyarwanda huyo anaweza kuvunja rekodi yake kwa kufunga mabao mengi msimu huu.

Mmachinga anashikilia rekodi ya kufunga mabao 26 kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara, huku mshambuliaji wa zamani wa Mtibwa Sugar, Abdallah Juma, alikaribia rekodi hiyo baada ya kufunga magoli 25 katika msimu wa mwaka 2014/15.

Kagere anaongoza katika orodha ya wafungaji wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu akiwa na mabao 19 akifuatiwa na Reliants Lusajo wa Namuungo, Yusuph Mhilu (Kagera Sugar) na Paul Nonga wa Lipuli, ambao kila mmoja ana magoli 11.

Akizungumza na Nipashe jijini Dar es Salaam jana, Mmachinga alisema uwezo wa mshambuliaji huyo wa Timu ya Taifa ya Rwanda ni mkubwa kwa sababu anajituma zaidi anapokuwa uwanjani.

Mmachinga alisema sababu ya kuamini Kagere ana nafasi ya kuvunja rekodi yake iliyodumu kwa muda mrefu ni baada ya kusikia mikakati iliyowekwa na benchi la ufundi la mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara ambalo linaloongozwa na Mbelgiji Sven Vandenbroeck.

"Mbali na mikakati ya benchi la ufundi la Simba katika kuhakikisha anafikia rekodi, sitaona ajabu Kagere kuvunja rekodi yangu iliyodumu kwa muda mrefu kwa sababu ni mtu wa kazi," alisema Mmachinga.

"Ni mchezaji ambaye anajitambua, ukiangalia huu ni msimu wa pili sasa anachukua tuzo ya ufungaji bora, kwa kasi yake nina imani ana uwezo wa kufunga mabao saba au zaidi katika michezo 10 iliyobakia," Mmachinga alisema.

Aliongeza atafurahi kuona rekodi yake inafikiwa na kuvunjwa, lakini furaha ingeongezeka zaidi kama mchezaji mzawa ndio 'angepokea kijiti' hicho kutoka kwake.

"Tatizo la wachezaji wetu wazawa wanashindwa kujitambua, kujitunza lakini pia wanaridhika mapema, msimu mmoja akichukua ufungaji basi msimu ujao hafikishi hata idadi ya mabao 10, hivyo ukiangalia kwa Kagere unaona jinsi anavyoweza 'kuwatesa' wazawa kwa misimu miwili mfululizo," alisema Mmachinga.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live