Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mlinzi wa Salah atoa siri hii..!

Salah Mlinzi.jpeg Mlinzi wa Salah atoa siri hii..!

Mon, 16 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mlinzi binafsi wa Nyota wa Misri Mohamed Salah, amezungumzia kazi yake ya kumlinda nyota huyo kutokana na mengi ikiwemo vitisho.

Karim Abdou amesema ”Salah ni maarufu Duniani lakini ni maarufu kupita kiasi nchini Misri kutokana na umahiri wake kwenye soka pamoja na kutoa misaada mbalimbali yenye thamani ya mamilioni nchini humo"

”Hatupendi kupokea zawadi kutoka kwa Mashabiki, lakini ikiwa tutazipokea huwa zinachekiwa na timu ya usalama ili kuhakikisha hazitomdhuru au kumuua.”

Mlinzi huyo ameeleza mengi katika mahojiano ya hivi karibuni kupitia Podcast ya 5ASide.

”Huyu ni kama mzimu, hawezi kuonekana, kuna siku alienda kusali Msikitini, hakuna mtu aliyejua kuwa alikuwa akiishi pale, mtu mmoja alimfuata na kuweka kwenye kundi la WhatsApp kuwa Mo Salah anaishi kwenye anuani hii”

"Baada ya muda mfupi tu , takribani watu 20,000 walifika na kujaa."

"Lakini aliposhinda Ligi ya Mabingwa huo ndio ulikuwa wakati mgumu kuliko yote”

”Ilikuwa Eid na kulikuwa na maelfu ya watu, alitakiwa kwenda mtaani kusali na wengine na ndio alikuwa ametoka kushinda Ligi ya Mabingwa kwahiyo kila mmoja alitaka kupiga naye picha”

”Media zote za Misri, Televisheni, magazeti yalijaa ilikuwa kama fainali ya Kombe la Dunia. Walikuwa wamejipanga nje ya nyumba yake".

”Hakuweza hata kufungua mlango, tulijaribu kumtorosha kupitia mlango wa nyuma, lakini ilishindikana”.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live