Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mlandege yatinga nusu fainali Kombe la Mapinduzi

MlandegeeeGrET.jpeg Mlandege yatinga nusu fainali Kombe la Mapinduzi

Mon, 8 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bingwa mtetezi Mlandege imeendelea kuweka hai matumaini yao ya kutetea ubingwa huo baada ya kuwatupa nje KVZ kwa matuta 3-2.

Dakika 90 za mchezo huo zilitamatika kwa timu zote kushindwa kupata bao huku zikicheza kwa kushambuliana kwa kasi lakini kukosa utulivu kutumia nafasi zao kulizigharimu timu zote.

Baada ya dakika 90 kumalizika hatua ya mikwaju ya penalti ilitumika kutafuta mshindi ambapo Mlandege ikaibuka kidedea kwa kupata ushindi wa penalti 3-2 KVZ watajilaumu wenyewe kwa kukosa penalti tatu za kwanza mfululizo huku Mlandege wao wakipata mbili za kwanza kisha kukosa ya tatu.

Matokeo hayo sasa yanaifanya Mlandege kusubiri mshindi kati ya Yanga dhidi ya APR mchezo ambao utapigwa saa chache zijazo kuanzia saa 2:15 usiku.

Mlandege ndio bingwa mtetezi wa taji hilo walipochukua taji hilo mbele ya Singida Fountain Gate msimu uliopita na sasa imekuwa timu ya kwanza kutinga hatua ya nusu fainali.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live