Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mlandege yapigwa kidude Ligi Kuu Zanzibar

Mlandege PBZ Mlandege yapigwa kidude Ligi Kuu Zanzibar

Thu, 2 Nov 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Bao pekee la Hafidh Barik Juma katika dakika ya 33 limeifanya Zimamoto kuizima Mlandege katika mfululizo wa mechi za Ligi Kuu ya Zanzibar (ZPL) iliyokamilisha raundi ya sita jana Novemba 1

Zimamoto ilipata ushindi huo kwenye mechi kali iliyopigwa Uwanja wa Mao A, mjini hapa na kuifanya timu hiyo ifikishe pointi nane na kuchupa kwa nafasi mbili kwenye msimamo wa ligi hiyo kutoka ya 11 hadi ya tisa ikiwa nyuma ya Mlandege iliyosaliwa na pointi 9 kila moja ikicheza mechi sita.

Hicho ni kipigo cha kwanza kwa Mabingwa wa michuano ya Kombe la Mapinduzi 2023 tangu katika ZPL kwa msimu huu na ushindi wa pili kwa Zimamoto.

Timu zote zilionyesha ufundi mwingi zikifanya mashambulizi makali ya hapa na pale ili kusaka mabao ya mapema, lakini umakini mdogo ulizifanya kila moja kupoteza nafasi za wazi hadi dakika ya 33, Hafidh alipowanyanyua mashabiki wa Zimamoto.

Bao hilo lilidumu hadi mapumziko na hata kipindi cha pili, licha ya timu zote kufanya mabadiliko ya wachezaji na kuongeza kasi ya mchezo, bado hakuna maajabu yaliyotokea kwani hadi dakika 90 zinatimia Zimamoto ilikuwa mshindi kwa bao hilo 1-0.

Ligi hiyo itaendelea tena Jumatano ya Oktoba 18 kwa pambano litakaloikutanisha Jamhuri dhidi ya JKU, mchezo utakaopigwa Uwanja wa FFU Finya. JKU itashuka uwanja huo wa ugenini ikitoka kuchezea kichapo cha mabao 3-0 ilichopewa jana Jumamosi na KVZ na kushushwa kutoka kileleni hadi nafasi ya pili.

KVZ ndio inayoongoza kwa sasa ligi hiyo ikiwa na pointi 16, tatu zaidi na ilizonazo JKU, huku Kipanga na Malindi zikifuata nyuma zikiwa na pointi 11 ila zinatofautiana mabao ya kufunga na kufungwa na watetezi KMKM ikifunga Tano Bora kwa kukusanya pointi 10 kama ilizonazo Chipukizi ya Pemba.

Chanzo: Mwanaspoti