Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mkwaya yazindukia kwa Yanga Princess

Kikosi Yanga Princess 1024x732 Yanga Princess

Sat, 18 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati Kocha Msaidizi wa Yanga Princess, Fred Mbuna akisema timu yake ilishindwa kufuata maelekezo vyema na kuambulia sare, Kocha Mkuu wa Mkwawa Queens, Damian Mussa, ametamba kikosi chake kimeamka na anatarajia kupata matokeo mazuri kwenye mechi zinazofuata.

Yanga Princess iliambulia suluhu dhidi ya Mkwawa Queens inayoburuza mkia katika Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania.

Mbuna alisema matokeo hayo yalitokana na wachezaji wake kushindwa kufuata maelekezo waliyowapa na kupoteza nafasi za kufunga mabao walizozipata.

"Tatizo ni wachezaji, wamecheza walivyoweza, tumepoteza nafasi nyingi ambazo tulizifanyia kazi mazoezini, hata hivyo hatujapoteza, tumepata suluhu, tutaenda kujipanga kwa ajili ya mechi nyingine. Hii ni ligi na mechi bado zipo nyingi, huwezi kusema tumepoteza matumaini ya kutwaa taji, bado tunaukimbiza ubingwa," alisema Mbuna.

Naye Mussa alisema kwa sasa wachezaji wake wameanza kuelewana na anaamini mchezo unaofuata watapata ushindi.

"Tumetoa sare na timu kubwa, nzuri inayocheza vizuri, sasa tumeanza ligi, kila timu itakayokuja mbele yetu, Fountain Gate Princess wanaosumbua tutakaocheza nao mechi ijayo wajiandae," alisema kocha huyo.

Simba Queens ndio vinara wa ligi hiyo wakiwa na pointi 26 sawa na Fountain Gate Princess, nafasi ya tatu inashikiliwa na JKT Queens yenye pointi 25 na Yanga Princess ipo kwenye nafasi ya nne ikiwa na pointi 21.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live