Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mkwawa Queens yalipa deni, yaachiwa

Mkwawa Queens Kikosi cha Mkwawa Queens

Sat, 18 Feb 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Siku moja baada ya Mwanaspoti kuchapisha taarifa za Mkwawa Queens kukwama katika moja ya hotel jijini Dar es Salaam ikidaiwa deni la Sh 810,000, hatimaye timu hiyo imepata msaada na kuachiwa huru.

Timu hiyo ya mkoani Iringa juzi ilijikuta iking’ang’aniwa Dar es Salaam kwenye moja ya hotel ilipokuwa imefikia kwa ajili ya mchezo wao wa ligi kuu ya Wanawake dhidi ya JKT Queens na kulala mabao 6-1.

Hata hivyo baada ya mchezo huo, timu hiyo ilijikuta matatani ikishikiliwa kutokana na deni hilo ikiwa ni gharama ya chakula, malazi na usafiri kwa kiasi hicho na kushindwa kusafiri kurudi nyumbani.

Ofisa habari wa timu hiyo, Francis Godwine amethibitisha timu hiyo kuachiwa baada ya kulipa deni hilo akiwashukuru wadau mbalimbali akiwamo Mkuu wa Mkoa huo, Halima Dendego.

“Ni kweli timu imeruhusiwa na muda wowote itakuwa nyumbani Iringa baada ya wadau akiwamo Mkuu wetu wa Mkoa kutuchangia, kwa ujumla tunawashukuru wadau wote,” amesema Godwine.

Godwine amesema kuwa changaomoto hiyo imewapa funzo akibainisha kuwa kwa sasa wakati wakienda kupumzika kwa takribani wiki mbili uongozi utaandaa mkakati kama walivyoelekezwa kuhakikisha wanaondokana na aibu hiyo.

Mkuu wa Mkoa huo, Halima Dendego amesema pamoja na kuichangia timu hiyo lakini msimamo wake ni uleule kuwataka viongozi wake kuandaa mkakati kuhakikisha wanaondoka na na kutembeza bakuli.

"Nimewaambia tena walete wadau wao kama walivyofanya Lipuli ili tuone tunaisaidiaje kuondoa hii aibu, lazima tubadilike tusonge mbele" amesema Halima.

Chanzo: Mwanaspoti