Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mkwawa Queens yakwama Dar kisa deni, yaiangukia TFF

Mkwawa Queens Mkwawa Queens yakwama Dar kisa deni, yaiangukia TFF

Sat, 18 Feb 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Pamoja na kukumbana na kipigo kizito jana cha mabao 6-1 dhidi ya JKT Queens, Mwakwa Queens hali imeendelea kuwa tete baada ya kukwama hotelini walipofikia Dar es Salaam wakidaiwa deni la Sh 810,000.

Timu hiyo ambayo ni msimu wake wa kwanza kucheza ligi kuu ya Wanawake, ndio wanaburuza mkia kwenye msimamo wa ligi hiyo kwa pointi moja baada ya kucheza mechi tisa.

Mkwawa Queens ya mjini Iringa ilikuwa na mechi yake ya kufunga raundi ya kwanza dhidi ya Maafande hao na kujikuta ikichakazwa kwa idadi hiyo ya mabao.

Ofisa habari wa timu hiyo, Francis Godwine amethibitisha timu hiyo kung’ang’aniwa hotelini walipofikia kuhakikisha wanalipa deni la Sh 410,000 ikiwa ni gharama ya chakula na malazi.

Pia amesema mbali na kiwango hicho, pia timu hiyo ina deni la gari la Sh 400,000 hivyo timu imeshindwa kusafiri kutoka Dar es Salaam kwenda mkoani Iringa.

“Tumewasiliana na Shirikisho la Soka nchini, (TFF) kuona namna ya kutusaidia kwa sababu katika pesa ya udhamini walishatupa Sh5 milioni wakati tunaanza japokuwa walituahidi jumla ya Sh25 milioni,” amesema Godwine.

Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Halima Dendego amesema bado hajapata taarifa hizo na kwamba huenda hata uongozi umeshindwa kumfikia kutokana na maelekezo aliyowapa kushindwa kuyatimiza.

Amesema mara kadhaa amekuwa sambamba na timu hizo kwani muda mwingine hujivunia uwapo wa timu hizo, lakini anahitaji kupata chimbuko kwani ameikuta timu ligi kuu.

“Haiwezekani kila mechi timu ichangiwe niliwaambia viongozi wawe na mpango mkakati kubuni vyanzo vya mapato lakini hadi sasa wako kimya, binafsi naumia kusikia hizo taarifa ila hata hivyo nataka kujua walioipandisha wako wapi,”

“Isije kuwa wanachangisha pesa wanaweka mifukoni mwao kila mtu kwa sasa ana shida na pesa, mimi kama kiongozi nimechangia sana hivyo nataka kujua msimamo wa timu hiyo haiwezekani Sh 810,000 iwasoteshe hivyo,” amesisitiza Dendego.

Chanzo: Mwanaspoti