Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mkwasa akazia pumzi kuiua Simba, Pablo ajipange

Ruvu Kirumba Ruvu Shooting

Wed, 17 Nov 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Kocha Mkuu wa Ruvu Shooting ametumia dakika 40 kusaka pumzi kwa wachezaji wake akiwapigisha zoezi la kukimbia kuzunguka nusu uwanja kwa raundi 20 wakijiwinda kuivaa Simba Ijumaa.

Timu iliwasili uwanjani hapo saa 9:30 alasiri na kuanza tizi saa 9:50 baadae, ambapo kabla ya kuanza mazoezi Mkwasa aliwaita nyota wake kati na kuwapa maelekezo akikadhia baadhi ya mambo baadaye wachezaji walianza na zoezi la kukimbia kuzunguka nusu uwanja taratibu mara tano na mazoezi mengine ya kurejesha utimamu wa mwili.

Baada ya hapo wakajigawa makundi mawili moja likiongozwa na Ally Mtoni (Sonso) na Pius Buswita likiwa na wachezaji 10 na lingine la akina Rashid Juma, Marcel Kaheza na wenzake lenye nyota tisa wakikimbia kuzunguka nusu uwanja mara 10 safari hii wakiongeza kasi kidogo.

Baada ya hapo aliwapumzisha kidogo wakaendelea tena na zoezi la kukimbia uwanja mara 10 kisha wakapata maji ya kunywa na kuhamia kwenye tizi la kuruka vihunzi akiwakazania spidi na umakini.

Mkwasa alitumia takribani dakika 40 kutafuta pumzi kwa wachezaji wake kwa kuwakimbiza jambo ambalo linaonekana ni mbinu za kukabiliana na Mnyama ili kikosi chake kisikate upepo mapema.

Baada ya zoezi la mbio, Mkwasa aliwaita kati na kuwapanga katika mafungu saba yenye wachezaji wanne ambapo walikuwa na zoezi la kupiga pasi unaachia unasogea kwenye nafasi.

Kikosi hicho kinaendelea na mazoezi uwanjani hapo chini ya Boniphace Mkwasa 'Master'.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz