Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mkwasa aipa mbinu Simba

B53db1f00d4feda7d9fbe7e26235364d Mkwasa aipa mbinu Simba

Sat, 9 Jan 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

KOCHA mkongwe Charles Mkwasa amesema kushambulia kwa kupitia pembeni ni mbinu wanayopaswa kutumia Simba kuwamaliza FC Platinum ya Zimbabwe kwenye mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika utakaopigwa keshokutwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Simba kwenye mchezo huo wanahitaji ushindi wa mabao kuanzia 2-0 ili kujihakikishia nafasi ya kusonga mbele katika hatua ya makundi baada ya kupoteza mchezo wa awali kwa bao 0-1 dhidi ya timu hiyo jijini Harare, Zimbabwe Desemba 23 mwaka jana.

Mkwasa ambaye ni kocha wa zamani wa Yanga na kwa sasa anakinoa kikosi cha Ruvu Shooting, alisema timu inayocheza kwa kujilinda muda wote kama FC Platinum inakuwa na uwezekana mkubwa wa kuzidiwa.

“Ndio maana wakitangulia kupata bao wanarudi nyuma wakiogopa kwenda mbele na kubaki kuziba nafasi na kucheza kwa makini kwa kupaki basi, huku wakiwaangalia wapinzani wao kama wakianza kuiga mbinu wanageuza kibao kwa kuanza kushambulia kwa kushtukiza.

“Ushauri wangu kwa benchi la Simba watumie mfumo wa kwenda kuwashambulia kupitia pembeni na hata kwenye mchezo uliopita Zimbabwe kwa njia hiyo walifanikiwa kuingia kwenye eneo hatari la Platinum na wakafanikiwa kupata bao, lakini walikuwa wameotea.”

Alisema kwanza wanatakiwa kucheza kwa kasi muda wote, lakini kushambulia kupitia pembeni ndio njia ya ushindi kwa urahisi kwani watawafanya wapinzani wao kuheza kwa presha kubwa na kufanya makosa.

“Kucheza kwa kutumia pembeni wapinzani inakuwa ngumu kuzuia krosi zinakuja kwenye eneo lao na kama Simba watafanya hivyo watafanikiwa kwa jinsi nilivyowatazama katika mchezo uliopita wataingia kwa kuwaangalia Simba,”alisema Mkwasa.

Mkwasa amewatahadharisha Simba wasije wakaingia kwenye aina ya mchezo wao, kwamba Platinum wataingia kwenye mechi hiyo wakijua wapinzani wao wanahitaji ushindi, hivyo watapooza mchezo na kuonekana kama hawana haraka.

“Simba watakuwa na nguvu kwakuwa watajaza mashabiki wao, lakini kwa makocha wenye akili wanaingia na mbinu ya kucheza mchezo wa taratibu hata kwa kutembea, wakimiliki mpira muda mrefu mashabiki watapoa, hawatakuwa na chakushangilia, “alisema.

Mkwasa aliyewahi kuinoa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ alisema anajua mbinu za kucheza na timu kubwa ndio maana Simba na Yanga wanapata shida wanapokutana na kikosi chake kupata matokeo.

Chanzo: habarileo.co.tz