Saa kadhaa baada ya kuthibitika ameachana na klabu ya Ruvu Shooting, Kocha mzawa Boniface Charles Mkwasa ametaja sababu ya kuachana na timu hiyo ambayo inashiriki Ligi Kuu Tanzania Bara.
Mkwasa alitangaza kuachana na Ruvu Shooting baada ya mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya KMC FC uliochezwa jana Jumanne (Desemba 28), Uwanja wa Azam Complex, Chamazi jijini Dar es salaam.
Timu hizo ziliagawana alama moja kila mmoja, kufuatia sare ya bao 1-1, huku Ruvu Shooting wakitangulia kupata bao la kuongoza, kabla ya KMC FC haijasawazisha dakika za lala.
Kocha Mkwasa amesema kilichomsukuma kuondoka Ruvu Shooting ni matokeo mabovu, tangu walipoanza msimu huu 2021/22.
“Nimeamua kuwajibika kutokana na kutotimiza malengo ya klabu.
umepitia changamoto nyingi hivyo nimeona ni vyema kuacha ili wengine waendelee pale nilipoishia,” amesema Mkwasa.
Kufuatia uamuzi huo wa Mkwasa, Kikosi cha Ruvu Shooting itaongozwa na Kocha Msaidizi, Rajab Nakuchema wakati uongozi ukiendelea kumsaka Kocha Mkuu kuchukua nafasi hiyo.