Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mkwabi, Rage wafunguka Simba SC

Rage Pic Data Mkwabi, Rage wafunguka Simba SC

Thu, 17 Dec 2020 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

By Imani MakongoroMore by this Author Dar es Salaam. Vigogo wa zamani wa klabu ya Simba, Swedi Mkwabi na Ismail Aden Rage wamefunguka kuhusishwa kugombea nafasi ya uenyekiti wa klabu hiyo kwenye uchaguzi mdogo unaotarajiwa kufanyika Februari 7, mwakani.

Rage na Mkwabi waliowahi kuwa wenyeviti wa klabu ya Simba kwa nyakati tofauti waliliambia gazeti hili jana kwamba licha ya baadhi ya wanachama kuwaomba wafanye hivyo, lakini hawana mpango huo.

Mkwabi ambaye alijiuzulu nafasi yake alisema,kurudi kugombea uongozi wa Simba ni mpaka mfumo wa klabu utakapobadilika.

“Ni kweli wanachama baadhi walinifuata kuomba nirudi, nikawaambia wangetaka nirudi wangehoji kwenye mkutano mkuu kwanini niliondoka na sio sasa, siwezi kurudi tena kwa kuwa sikujiuzulu kwa bahati mbaya.

“Hata mwenyekiti ajaye naamini atakuwa na kazi ngumu kama mfumo wa klabu hautabadilika, kwani kuongoza Simba tangu nimeingia mfumo haukuwa rafiki, unakuwa mwenyekiti usiye na nguvu, ni kama kuwa rais halafu hauna nguvu kwenye baraza la mawaziri,” alisema Mkwabi.

Chanzo: mwanaspoti.co.tz