Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mkuu wa Mkoa atangaza dau nono kuinusuru Tabora United

Vlcsnap 2024 05 21 21h19m48s036 1024x576.png Mkuu wa Mkoa wa Tabora Paul Chacha

Wed, 22 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Paul Chacha ametangaza rasmi kuanza kuiunga mkono timu ya Tabora United kwa kuipatia zaidi ya shilingi milion kumi kila inaposhinda mechi katika michezo mitatu iliyosalia kwenye ya ligi kuu ya NBC,

Chacha ametoa hamasa hiyo mapema leo alipoitembelea timu hiyo ambayo imepiga kambi ikijiandaa kuwakabili Ihefu SC mchezo unaotarajiwa kupigwa kesho Mei 22 kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora,

Tabora United ambao wako nafasi ya 14 wakiwa na alama 26, wanakabiliwa pia na mechi dhidi ya Yanga pamoja na Namungo FC zote ugenini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live