Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mkutano wa Eto'o na kocha wa Cameroon wageuka kuwa vurugu

Etoo Na Brys Eto'o na Brys.

Wed, 29 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Video iliyosambazwa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii na iliyochukuliwa na waandishi wa habari, inamuonyesha Eto'o akimkaribisha kocha huyo mpya wa Cameroon japo baadaye, mkutano huo uligeuka kuwa uwanja wa kurushiana cheche za maneno.

Huo ulikuwa ni mkutano wa kwanza kati ya Eto'o na Brys ambaye aliteuliwa na wizara ya michezo nchini humo kama kocha wa timu ya taifa bila ya ridhaa kutoka shirikisho la soka la Cameroon.

Hatua hiyo inatajwa kuwa chanzo cha mgogoro kati ya wawili hao. Shirikisho la soka nchini humo FECAFOOT inatarajiwa kutoa taarifa hapo baadaye kuhusu tukio hilo.

FECAFOOT ilielezea nia ya kufanya kazi na Mbelgiji huyo licha ya awali kukosoa uteuzi wake na kuutaja kama uamuzi wa mtu mmoja tu uliochukuliwa na Waziri wa michezo Narcisse Mouelle Kombito.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live