Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mkutano Mkuu Yanga kufanyika Juni 27

8ad6a997bc57c6e018c1457b4ce75cbf.png Mkutano Mkuu Yanga kufanyika Juni 27

Sat, 22 May 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

KLABU ya Yanga inatarajiwa kufanya mkutano wake mkuu wa mwaka Juni 27 kwa mujibu wa ibara ya 20 ya katiba yao ili kujadili mambo mbalimbali yanayowahusu.

Huu unakuwa mkutano mkuu wa kwanza katika kipindi cha miaka miwili ya uongozi wa Mwenyekiti wa klabu hiyo, Profesa Mshindo Msola, ambaye alichaguliwa kukalia kiti cha uongozi Mei 5, 2019.

Msola pamoja na Kamati ya Utendaji ya timu ya Yanga wameamua kufuata katiba yao kwa kukutana na wanachama ili kuweka wazi maendeleo ya timu pamoja na mipango yao ya msimu huu na msimu ujao.

Kamati ya Utendaji ya timu hiyo inatoa wito kwa wanachama kulipia kadi kwa mwaka mmoja kama ambavyo uongozi ulivyotoa maelekezo hapo awali.

Akizungumza na gazeti hili Ofisa Habari wa timu hiyo, Hassan Bumbuli alisema kwamba wanachama wa Yanga wanapaswa kufanya maandalizi ya kuhudhuria mkutano huo sasa kwa kulipa ada za uanachama wao mapema,

Katika mkutano huo ukaguzi mkubwa utafanyika kabla ya watu kuingia ndani ya ukumbi.

“Mkutano utafanyika Juni 27, wanachama wenye kadi ambazo hazijalipiwa wanapaswa kuhakikisha wanalipia mapema muda uliopo unatosha ili kupata haki ya kuhudhuria mkutano huu,”alisema Bumbuli.

Chanzo: www.habarileo.co.tz