Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mkude ni majeruhi, Pacome, Lomalisa kukiwasha kesho - Walter

Lomalisa Pacome Mkudee Mkude, Pacome na Lomalisa.

Tue, 30 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kuelekea mchezo wa robo fainali ya Kombe la Shirikisho la CRDB dhidi ya Tabora United, Kikosi cha Wananchi Young Africans kimeendelea na mazoezi baada ya mchezo wa weekend iliyopita wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Coastal Union.

Akizungumza kuhusu maandalizi ya kikosi hicho kuelekea mchezo huo, Meneja wa Kikosi cha Yanga, Walter Harriosn amesema kuwa juzi walifanya mazoezo mepesi ya kurejesha utimamu wa mwili na jana yameendelea mazoezi ya kawaida na kimbinu kabla ya kuhitimisha mazoezi hayo leo na kesho kukipiga na Tabora katika Dimba la Azam Complex majira ya saa 2:30 usiku.

“Kikosi kizima kinaendelea vizuri na kwa kiasi kikubwa wachezaji wako vizuri isipokuwa Jonas Gerard Mkude ambaye amepata majeraha ya mguu na anaendelea kupata matibabu. Joyce Lomalisa na Pacome Zouzoua wanaendelea vizuri na mazoezi na ikimpendeza mwalimu watakuwa sehemu ya mchezo wa kesho.

Aidha, walter amewataka mashabiki Wananchi wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuwapa sapoti wachezaji wao kuelekea kwenye malengo ambayo wamejiwekea msimu huu wa kutwaa ubingwa wa makombe yote ambayo walikuwa nayo msimu uliopita.

“Tuko vizuri, na tuko tayari kwa mapambano. Tunaamini tutakwenda kuandika historia nyingine ya kutetea makombe haya kwa msimu wa tatu mfulululizo. Wananchi njooni mtupe sapoti tuandike historia pamoja,” amesema Walter.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live