Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mkude atakiwa kulipa Sh milioni 2

283f1ae2038ee43d35f6fe0b828f1b64 Mkude atakiwa kulipa Sh milioni 2

Mon, 25 Jan 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

KAMATI ya Nidhamu ya Klabu ya Simba chini ya mwenyekiti wake, Suleiman Kova imemtoza faini ya Sh milioni 2 mchezaji wa timu hiyo, Jonas Mkude kwa kosa la utovu wa nidhamu.

Mkude amepatikana na hatia ya makosa matatu, ikiwamo kutohudhuria semina ya benchi la ufundi, ambapo adhabu yake anatakiwa alipe Sh milioni 1, kuchelewa kungia kambini wakati timu ilipokuwa ikijiandaa na mchezo dhidi na Coastal Union. Kosa hilo atalipa Sh milioni 1, huku pia amewekwa katika kipindi cha uangalizi cha miezi sita.

Kova alisema Mkude hakukutwa na hatia katika shtaka la kutoripoti kambini Desemba 26, 2020 bila ruhusa kwani hakukuwa na ushahidi wa kutosha.

Kamati hiyo imemtaka Mkude kurejea kambini mara moja kuendelea na mazoezi na asipofanya hivyo atakuwa amefanya tena kosa la utovu wa nidhamu, huku faini alizotozwa akitakiwa kulipa ndani ya mwezi mmoja.

Pia Mkude ametakiwa na kamati hiyo kuomba radhi mara moja ndani ya saa 24 tangu ilipotolewa hukumu hiyo.

Chanzo: habarileo.co.tz