Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mkude atakiwa kujipa angalizo

Mkude Pic Data Mkude atakiwa kujipa angalizo

Tue, 5 Jan 2021 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

By Oliver AlbertMore by this Author Dar es Salaam. Kiungo wa Simba, Jonas Mkude anatakia kujitathimini, kubadilika na kutambua kuwa yeye ni kioo cha wachezaji chipukizi, hivyo utovu wa nidhamu utamuharibia kipaji chake.

Uongozi wa Simba ulimsimamisha Mkude juzi kwa muda usiojulikana kutokana na makosa ya utovu wa nidhamu ambayo hayakuwekwa wazi.

Licha ya Simba kutoanika utovu huo wa nidhamu wa Mkude, lakini mchezaji huyo amekuwa na mfululizo wa kukumbwa na matukio mbalimbali na hivyo kujikuta midomoni mwa wadau wa soka.

Jun, 2019 aliingia matatizoni na kocha wa Taifa Stars, Emmanuel Amunike, ambaye alimtema katika kikosi chake kilichokuwa kikijiandaa na mchezo wa kirafiki dhidi ya Misri uliofanyika Juni 13, 2019.

Amunike alimua kumtema Mkude katika kikosi chake baada ya kushindwa kuhudhuria mazoezi, huku ikidaiwa kuwa alidai ameomba apumzike kwani alichoka kutokana na kucheza mechi nyingi na mfululizo akiwa na klabu yake ya Simba.

Chanzo: mwanaspoti.co.tz