Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mkude ana rekodi zake NBC Premier Ligue

Jonasmkude20 1692954340145 (1).jpeg Mkude ana rekodi zake NBC Premier Ligue

Mon, 15 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jonas Gerald Mkude, moja ya wachezaji wakongwe waliosalia kwenye NBC Premier League na ni mchezaji pekee mzawa kwa sasa ambaye ameitumikia Simba SC na sasa ‘anakipiga’ pale mitaa ya Jangwani.

Katika mechi nne za hivi karibuni za Yanga, Mkude ameanza kwenye michezo mitatu na mmoja kuanzia kwenye benchi kisha kuingia mchezoni.

Mkude alianza kwenye mechi zote mbili za robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Mamelodi Sundowns, mechi ya CRDB Bank Federation Cup dhidi ya Dodoma Jiji, Mkude aliingia kipindi cha pili.

Mechi ya jana ya NBC Premier League dhidi ya Singida Fountain Gate, Jonas Mkude alicheza dakika 85, kisha akatoka na nafasi yake kuchukuliwa na Zawadi Mauya.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live