Swali kubwa kwa mashabiki baada ya kusikia tetesi za Jonas Mkude kusaini Yanga, ni nini kitatokea kikosini haswa kwenye eneo la kati anapokwenda kucheza akikutana na mastaa waliotamba msimu uliopita na kujitengenezea ufalme mbele ya mashabiki.
Je, yule namba 6 aliyekuwa akimsema Ofisa Habari wa Yanga, Ali Kamwe ndiyo Mkude? Je, kati ya Khalid Aucho na Yanick Bangala nani atakwenda benchi?
Ni suala la muda, lakini habari za ndani zinasema kwamba Yanga huenda wakapumua kama Mkude ataweza kuwa kwenye ubora wake kwani Bangala tayari walishaanza kumtafutia mbadala kutokana na kiwango chake pamoja na mengine ya nje ya uwanja. Kocha Gamondi, anaweza kuanza na Mkude na Aucho katikati.