Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mkude afunguka magumu aliyopitia Simba

Mkude Simba Ss Mkude afunguka magumu aliyopitia Simba

Tue, 27 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Aliyekuwa kiungo wa Simba, Jonas Mkude amefunguka magumu aliyopitia ndani ya Klabu hiyo ambayo ameitumikia kwa miaka 13 tangu alipojiunga akiwa mdogo.

Mkude ambaye ameachana na Yanga wiki iliyopita, kupitia kipindi cha Jahazi cha Clouds FM, amesema kuwa alipata wakati mgumu pale alipokosa namba kwenye kikosi cha kwanza cha Msimbazi.

"Moja ya nyakati zangu ngumu ndani ya Simba ni kutocheza katika kikosi cha (1). Hakuna mchezaji ambaye atakuwa nje na atafurahia kutocheza. Binafsi iliniuma sana.

"Hiki kilikuwa kipindi kigumu zaidi kwangu na kocha alikuwa na machaguo mengine na mimi sikuwa na majeraha.

"Siwezi kuisema Simba vibaya. Kuhusu Thank You wadau wasitoe lawama kwa klabu kwani nafahamu Klabu inatambua mchango wangu. Ni mapema kusena naenda wapi japo simu zinaita sana (Akacheka)," amesema Jonas Mkude.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live