Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mkude aenguliwa kikosi cha Stars

Jonas Mkude Straz Kiungo wa Taifa Stars, Jonas Mkude

Tue, 5 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo wa Timu ya Taifa Jonas Gerald Mkude ameomba kuondolewa katika kikosi cha Timu ya taifa ya Tanzania "Taifa Stars" ambacho kimeitwa ili kuingia kambini siku chache zilizopita na Kocha Kim Poulsen.

Taifa Stars inajiandaa na mchezo dhidi ya Benin Oktaba 7, kuwania kufuzu kwa Fainali za Kombe la Dunia Qatar 2022.

Akizungumzia Sakata hilo, Meneja wa Stars Nadir Haroub Cannavaro amesema Kiungo huyo alifika mpaka kambini na amezungumza na Mwalimu na kumueleza shida yake na mwalimu amemruhusu hivyo ni rasmi itamkosa mchezaji huyo.

Sababu zinazotajwa kumuondoa Mkude Stars ni sababu za kifamilia.

Wiki chache zilizopita, Jonas Mkude alimpoteza mtoto wake hivyo inaonekana ni miongoni mwa mambo yaliyochangia kuomba aenguliwe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live