Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mkude Simba, Mkude Yanga!

Mkude Simba Ss Mkude Simba, Mkude Yanga!

Wed, 28 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Hata kama hatasajiliwa na Yanga au atasajiliwa. Mashabiki mjue mpira wa sasa ni ajira sio mpira mapenzi.

Kwa utafiti wangu mdogo niliofanya kupitia mitandao mbalimbali, nimebaini kuwa.

Mashabiki wa Simba na Yanga wamegawanyika kuhusu kuhusishwa kwa, Jonas Mkude kujiunga na Yanga.

Baadhi ya mashabiki wa Yanga wanasema, Mkude wa nini? akisajiliwa watahama timu. Wengine wanasema, Mkude ataongeza kitu, hata asipoanza 1st eleven lakini ataongeza ubora kwenye benchi ambapo itafanya ndani ntinti na nje ntinti.

Baadhi ya mashabiki wa Simba SC wanasema itawauma sana kumuona mchezaji wao kipenzi anaenda Yanga, viongozi wafanye iwezekanavyo asiende. Wengine wanasema mpira ni maisha, mwache aende akatafute.

Mashabiki wote wanaweza kuwa sahihi kulingana na hisia zao kwa mchezaji. Binadamu hawalingani jinsi ya kupokea jambo hasa linalohusisha hisia.

Lakini wote kwa pamoja wanapaswa kujua kwamba, Soccer ni AJIRA ya muda mfupi. Kila mchezaji angependa kupata pesa katika muda huo mfupi kadri inavyowezekana.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: