Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mkude, Ntibazonkiza waongeza mzuka Simba

Mkude Saidoo Mkude, Ntibazonkiza waongeza mzuka Simba

Fri, 17 Feb 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Baada ya kukosekana kwenye mchezo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Horoya, mastaa wa Simba, Jonas Mkude na Saido Ntibazonkiza ni sehemu ya wachezaji waliokuwa kwenye mazoezi leo asubuhi.

Simba leo asubuhi imefanya mazoezi yake ya mwisho asubuhi wakijiandaa na mchezo wao wa kesho dhidi ya Raja Casablanca.

Mkude awali mara ya mwisho kuonekana kwenye kikosi cha Simba ni katika mechi za kirafiki nchini Dubai lakini leo alikuwa sehemu ya kikosi cha Simba kinachojiandaa na mchezo wa kesho.

Upande wa Ntibazonkiza yeye alikosekana kwenye mchezo dhidi ya Horoya kwa kile kilichoelezwa alipata maumivu ya nyanya za paja.

Wakati Mkude akirejea,mkongwe Erasto Nyoni amekosekana katika mazoezi hayo.

Wachezaji hao licha ya kukosekana kwenye mchezo wa kwanza lakini katika mazoezi ya jana walionyesha kuwa fiti.

Mkude alikuwa imara kwa kila zoezi lililokuwa linatolewa na kama ikitokea shida kwenye eneo la kiungo basi kazi ni kwa Robertinho kumpa nafasi.

Upande wa Ntibazonkiza yeye alikuwa imara lakini kwenye mguu wake wa kulia eneo la kigimbi alikuwa ameweka plasta.

Urejeo wa Ntibazonkiza unaongeza kitu kwenye eneo la ushambuliaji ambalo mechi ya kwanza walipata nafasi nyingi na kushindwa kuzitumia.

Simba mchezo wa kwanza dhidi ya Horoya uliyochezwa nchini Guinea walifungwa 1-0 na sasa wana nafasi ya kujitetea uwanja wao wa nyumbani katika mchezo wa kundi C dhidi ya Raja.

Chanzo: Mwanaspoti