Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mkude, Mauya na Ngushi wameiangusha Yanga - Master Tindwa

Mkude, Mauya, Ngushi . Mkude, Mauya na Ngushi wameiangusha Yanga - Master Tindwa

Mon, 8 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi wa soka Bongo, Master Tindwa amesema, kwenye mechi ya Robo Fainali ya Kombe la Mapinduzi, Mkude, Mauya na Ngushi ndio walioiangusha timu ikapoteza kwa 3-1.

Amesema, nyota wengine walipambana sana kuipigania nembo ya Yanga.

“Mshery alikuwa nje muda mrefu hajacheza lakini kiwango alichoonesha anaonekana kabisa huyu ana kitu. Nanguka pia alikuwa na game nzuri sana na mwingine ni Shekhani hata alivyoingia aliongeza kitu.

“Wachezaji hawa wamepewa nafasi na wameonesha wanakitu, Yanga itaangalia inawatumiaje. Lakini kuna wachezaji wazoefu kama Ngushi, Mauya na Mkude wameiangusha Yanga kwa kweli.

“Ukiacha magoli mawili aliyofunga mechi ya kwanza, mechi zingine ameonesha kwanini anakaa nje na Mashabiki wamepata majibu kwanini hawa wanakaa nje,” amesema Master Tindwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live