Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mkude, Kennedy ndani, Simba ikiwavaa Namungo

FDRyr5mXoAItZIQ (600 X 726) Kikosi cha Simba dhidi ya Namungo

Wed, 3 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wekundu wa Msimbazi na Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu wanashuka dimbani kwa Mkapa majira ya saa 1:00 usiku kusaka alama tatu mbele ya Namungo.

Simba ambayo wameanza Ligi kwa kusua sua msimu huu wamecheza michezo minne na kushinda miwili tu.

Katika mchezo huo wa leo jina la kiungo Jonas Mkude limeonekana katika wachezaji watakaoanza mechi ya leo.

Halikadhalika beki Kennedy Juma pia amepata nafasi ya kuanza akichukua nafasi ya beki Henock Inonga mwenye adhabu ya kadi nyekundu.

Jina la beki aliekuwa akifikirisha watu pia, Paschal Wawa lipo kwa wachezaji wa akiba.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live