Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mkongwe Simba amvulia Kofia Yao

Pwasa X Yao Kuassi Mkongwe Simba amvulia Kofia Yao

Wed, 16 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mlinzi wa Kkulia wa Yanga Yao Kouassi ameendelea kuwakamata wadau wengi wa soka kutokana na kiwango chake alichokionesha katika michezo michache aliyocheza.

Mchezaji wa zamani wa Simba amefunguka kuhusu mchezaji huyo;

Huyu beki ana mapafu ya mbwa! Ndiyo kauli ya nyota wa zamani wa Simba, Shekhan Rashid akimmwagia sifa beki mpya wa pembeni wa Yanga, Kouassi Attohoula Yao akiamini Wana Jangwani wamepata mtu huku akimlinganisha ubora na beki wa zamani wa Wekundu wa Msimbazi, Boniphace Pawas . “Kouassi kaja kweli kufanya kazi ni bonge la mchezaji, jamaa ana energy (nguvu) dakika zote 90, hapa watani wamepata ubavu wa maana sana, yuko sawa anakupa vyote kwenye kushambulia na kuzuia pia, touch yake tu unajua huyu mchezaji, ananikumbusha enzi za Pawasa (Boniphace) kasoro tu hawachezi nafasi moja” . “Lakini pia huyu beki ana ‘mapafu ya mbwa’. Kwa jinsi ambavyo nimemuona mechi dhidi ya Azam kuanzia dakika ya kwanza nguvu na pumzi aliyokuwa nayo ndiyo hiyo hiyo ambayo amemaliza nayo mechi, inaonekana ni mchezaji ambaye yupo fiti, anajitunza na anafuata misingi ya soka,” alisema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live