Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mkomola asaka namba Stars

42ca92a4ec9b3f02af8e32ce93212995 Mkomola asaka namba Stars

Mon, 12 Oct 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

MCHEZAJI wa klabu ya Inglets FC ya Ukraine, Yohana Mkomola amesema anapambana kutafuta fursa ya kuitwa kwenye kikosi cha timu yaTaifa, Taifa Stars.

Akizungumza kwa njia ya mtandao jana, Mkomola ambaye timu yake inashiriki Ligi Kuu ya Ukraine, alisema kitendo cha kutokuitwa kwenye kikosi cha Stars kilichocheza mechi ya kirafiki na Burundi jana ni changamoto kwake.

“Kila mchezaji anayecheza nje ya nchi ana ndoto ya kulitumikia taifa lake, najua kocha anafuatilia ninachokifanya hivyo naendelea kupambana sehemu nilipo kuona naitwa safari nyingine,” alisema.

Mkomola ni miongoni mwa wachezaji waliounda kikosi cha timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys, kilichoshiriki michuano ya Afcon Gabon mwaka 2017.

Aliwatakiwa kila la kheri wachezaji walioitwa kwenye kikosi hicho, akiamini watafanya makubwa kwa kupata ushindi utakaorudisha heshima kwa taifa na mashabiki.

Mkomola tangu asaini mkataba wa kuitumikia timu hiyo mwanzoni mwa mwaka huu amekuwa akianza kikosi cha kwanza kwenye mechi za ligi hiyo inayoshirikisha timu 14.

Inglets inashika nafasi ya 10 kwenye msimamo baada ya kucheza mechi tano, wakiwa na pointi tatu, wakishinda mechi moja na kupoteza nne.

Chanzo: habarileo.co.tz