Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mkiani ligi ndiyo imeanza upyaaa

Adam Adam.jpeg Mshambuliaji wa Ihefu, Adam Adam

Tue, 7 Feb 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Matokeo ya ushindi kwa timu tatu zilizokuwa nafasi ya chini kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara katika mechi za juzi yameongeza presha katika vita ya kupambana kukwepa kushuka daraja na kufanya hesabu kuanza upya.

Katika mechi za wikiendi iliyopita ilishuhudiwa Ihefu ikiwa nyumbani ikiendeleza ushindi kwa kuipopoa Mbeya City mabao 2-0 na kuchumpa nafasi ya saba kwa pointi 26.

Ruvu Shooting wakicheza mara ya kwanza kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro waliibamiza KMC kwa mabao 2-1 na kujinasua mkiani wakifikisha pointi 17.

Nao Dodoma Jiji wakiwa nyumbani waliikandika mabao 2-1 Azam FC na kupanda nafasi ya 11 kwa pointi 24 na sasa kazi imebaki kwa Polisi Tanzania walio mkiani ambao jana walikuwa kibaruani dhidi ya Kagera Sugar.

Hata hivyo, matokeo hayo yalionekana kuziathiri KMC na Tanzania Prisons zilizoshuka nafasi za chini ikiwa ni 12 na 13 baada ya kupoteza na kutoka sare kwenye mechi zao.

KMC ilipoteza mbele ya Ruvu Shooting huku Prisons ikilazimishana suluhu na Mtibwa Sugar ikiwa ni mechi ya kwanza kwa kocha wake mpya, Abdalah Mohamed ‘Bares’.

Kocha mkuu wa Ihefu, Zuberi Katwila alisema kwa sasa wanaona matumaini mapya kwani hali ilikuwa mbaya, lakini presha inaanza kupungua kutokana na matokeo.

“Kimsingi bado tunahitaji ushindi zaidi ili kujiweka sehemu nzuri zaidi na kubaki salama Ligi Kuu msimu ujao,” alisema Katwila.

Chanzo: Mwanaspoti