Mwanasoka wa Kenya, Clarke Oduor amekamilisha uhamisho katika klabu ya Bradford City nchini Uingereza.
Klabu hiyo inayoshiriki Ligi ya Pili ya soka ya Uingereza ilitangaza usajili wa beki huyo mwenye umri wa miaka 23 siku ya Jumanne kupitia tovuti yake rasmi.
"Msajili wetu ya kwanza iko kwenye jengo. Karibu kwa mchezaji wa kimataifa wa Kenya Clarke Oduor ambaye anawasili kwa mkataba wa miaka mitatu,” taarifa ya Bradford ilisoma.
Clarke Oduor alisajiliwa kutoka klabu nyingine ya Uingereza, Barnsley ambayo inashiriki katika League One. Kiasi cha pesa ambacho uhamisho wa beki huyo chipukizi uligharimu hata hivyo hakijafichuliwa.
Oduor alisema alifurahishwa na changamoto yake mpya na akathibitisha yuko tayari kwa kazi iliyo mbele yangu.
"Siwezi kusubiri kuanza changamoto yangu mpya katika Bradford City! Klabu kubwa inayokwenda katika mwelekeo sahihi na mwanzo mpya kwangu kuonyesha kila mtu ninachoweza kufanya," alisema.
Aliongeza, "Nimefurahi sana kucheza mbele ya mashabiki kwenye Valley Parade na kujitolea kwa ajili yao!"
Clarke Oduor hachezi tu kama mlinzi lakini pia anaweza kucheza kama winga. Alihitimu kutoka akademi ya soka ya Leeds United mwaka wa 2017 kabla ya kujiunga na South Yorkshire mwaka wa 2019 na baadaye Barnsley.
Siye Mkenya pekee anayecheza Ulaya kwa sasa.
Katika miaka ya hivi majuzi, idadi nzuri ya wachezaji chipukizi wa Kenya wamejiunga na akademi za EPL. Wao ni pamoja na;
• Aymen Onyango: Man City (2023 na miaka 9.
• Leo Messo alijiunga na Arsenal 2021 na miaka 10.
• George Gitau alijiunga na Middlesbrough 2020 na miaka 16.
• Brooklyn Kazungu alijiunga na Leicester 2017 na miaka 9.
• Zech Obiero alijiunga na Tottenham 2015 na miaka 8.
• Tyler Onyango alijiunga na Everton 2011 na miaka 8.
• Clarke Odour alijiunga na Leeds 2010 na miaka 10.
• Silko Thomas alijiunga na Chelsea tarehe isiyothibitishwa.