Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mkenya aipa saluti Ligi Kuu Bara

Gacsfcf Mkenya aipa saluti Ligi Kuu Bara

Tue, 13 Feb 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Kocha Mkuu wa Dodoma Jiji, Francis Baraza amesema Ligi Kuu Bara ni bora kuliko ya Kenya (FKFPL) kuanzia kwenye ushindani hadi uwekezaji.

Baraza ametua ndani ya kikosi hicho huku akiwahi kuzifundisha timu mbalimbali zikiwemo Sony Sugar, Chemelil Sugar na Kenya Police za nchini Kenya, ilhali Bongo alizifundisha Biashara United, Kagera Sugar na sasa Dodoma Jiji.

“Mimi nimefundisha timu tano Kenya, pia tatu hapa Tanzania, ila huku kuna ushindani na ubora sana kwa sababu hata mwamko wa mashabiki ni mkubwa. Hata bonasi za hapa ni nzuri hivyo acha nikiri wazi maisha mazuri yapo ya mpira huku,” alisema Baraza

Kocha huyo aliyeiongoza Dodoma katika mechi tatu, akishinda moja, sare moja na kupoteza moja ambapo ameeleza malengo yao ni kumaliza nafasi za juu akiainisha mabadiliko madogo waliyofanyha dirisha dogo la Januari yataanza kuwalipa hivi punde.

“Wapo wachezaji wa kigeni ambao wamekuwa hawaonekani kwa sababu ya vibali ya kufanya kazi nchini vinashughulikiwa, hivyo niwatoe hofu mashabiki wetu kwa kuwaambia tupo imara na waendelee kutupa sapoti kwa sababu tunawategemea wao.”

Timu hiyo inashika nafasi ya saba na pointi 19 baada ya kucheza michezo 15 ambapo kati yake imeshinda mitano, sare nne na kupoteza sita.

Chanzo: Mwanaspoti