Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mke wa Dani Alves amaliza utata

Dan Alives Pic Mke wa Dani Alves amaliza utata

Wed, 8 Feb 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Mke wa mwanasoka, Dani Alves mrembo Joana Sanz amemtembelea mumewe gerezani kwa mara ya kwanza tangu alipofungwa kwa madai ya kubaka.

Mrembo, Joana, 29, ambaye ni mwanamitindo - alitumia dakika 50 ndani ya jela alilomo Alves na baadaye alisema: “Siwezi kumwacha pekee yake katika kipindi hiki kigumu katika maisha yake.”

Joana aliamua kueleza bayana sapoti anayompa mumewe ikiwa ni siku chache tangu zilipoibuka taarifa kwamba alidai talaka na Alves aligoma kuonekana naye alipokwenda kumtembelea gerezani.

Joana alisema vyote vilivyoelezwa nyuma ni uongo tupu, akisisitiza kwamba yeye na mumewe bado wapo vizuri na atakuwa naye bega kwa bega katika nyakati hizi ambazo staa huyo wa Kibrazili akishutumiwa kubaka alipokuwa kwenye kumbi moja ya starehe za usiku huko Barcelona. Mrembo Joana alisema:

“Taarifa za kwamba Alves aligoma kukutana na mimi wiki iliyopita ni uongo. Niko vizuri sana, nashukuru.” Alimalizia alipoulizwa jinsi anavyojisikia baada ya kumwona Alves akiwa gerezani.

Joana alitembelea gerezani akiwa na mpishi Bruno Brasil, ambaye inaripotiwa alikuwa pamoja na Alves katika usiku ambao kuna mwanamke alidai kubakwa na gwiji huyo wa Barcelona huko kwenye kumbi moja ya starehe za usiku inayoitwa Sutton.

Alves, 39, alikiri mbele ya polisi kushiriki ngono na mwanamke huyo, lakini alikataa madai ya kwamba alimbaka. Alves amewekwa tangu tangu Januari 20.

Chanzo: Mwanaspoti