Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mke wa Casemiro amtetea mume wake kufuatia kichapo cha 3-0

Mke Wa Casemiro Amtetea Mume Wake Kufuatia Kichapo Cha 3 0.png Mke wa Casemiro amtetea mume wake kufuatia kichapo cha 3-0

Tue, 3 Sep 2024 Chanzo: Bbc

Kipigo cha Manchester United cha 3-0 nyumbani dhidi ya Liverpool kilikuwa uchungu sana kwa kiungo wa kati wa Brazil, Casemiro, ambaye alitolewa wakati wa mapumziko kisha akakosolewa na wachambuzi.

Kulikuwa na madai kwamba aliondoka Old Trafford wakati wa mapumziko, lakini mkufunzi wa United Erik ten Hag alikanusha hili.

Sasa mke wake Casemiro amemtetea mumewe, na kuwakumbusha watu mataji mengi ambayo ameshinda katika maisha yake yote ya soka.

Anna Mariana alituma picha ya mkusanyiko wake wa mataji alioshinda kwenye Instagram, huku Mbrazil huyo akiwa ameshinda Ligi ya Mabingwa mara tano pamoja na La Liga mara tatu akiwa na Real Madrid na, hivi majuzi, Kombe la FA akiwa na Manchester United.

Kisha alichapisha picha ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32 akisherehekea na wenzake akiandika: "Daima hodari Casemiro, mkubwa zaidi (akiweka emoji ya moyo).

"Casemiro alifanya makosa mawili katika dakika 45 za kwanza kwenye mchezo wa Jumapili Uwanjani Old Trafford, ambapo Liverpool walifunga bao katika ushindi wao mnono.

Beki wa zamani wa Liverpool Jamie Carragher alisema kwenye Sky Sports: "Ni jambo la kusikitisha kuona anachopitia huko nje."

"Lazima niseme amepoteza kujiamini kidogo," aliongeza beki wa zamani wa Manchester United Gary Neville.Nafasi ya Casemiro ilichukuliwa wakati wa mapumziko na Toby Collyer, 20, ambaye alicheza mechi yake ya kwanza United.

Akielezea uamuzi wake, Ten Hag alisema: "Tulilazimika kufanya uamuzi mgumu kwa sababu tulitaka kusawazisha, halafu unahitaji wachezaji kwenye safu ya kati ili kuzuia wapinzani, kwa hivyo tukamweka Toby Collyer uwanjani."

Nadhani katika soka kila mtu anatakiwa kuwajibika.

Nina hakika ni mtu mwenye tabia nzuri na alishinda kila kitu katika maisha yake ambayo unaweza kufikiria.

Nina hakika ataendelea kuchangia timu yetu na Casemiro ni mshindi kila siku hivyobasi ataendelea kuwepo."

Chanzo: Bbc