Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mkataba wa Saido unasema lazima aanze kikosi cha kwanza

Saido Kuwasili.jpeg Saido Ntibazonkiza

Thu, 11 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Taarifa kutoka chanzo kilicho karibu na kiungo mshambuliaji wa Simba, Saido Ntibazonkiza zinaeleza kuwa, mkataba wa mchezaji huyo una kipengele cha kwamba lazima aanze kwenye kikosi cha kwanza cha Simba.

Kumekuwa na maneno mengi kutoka kwa mashabiki wakihoji kuwa, kwa nini kocha Benchikha amekuwa akimpanga kila mechi licha ya kuonesha kiwango kibovu na kukosa mabao ya wazi?

"Katika makubaliano ya kimkataba kati ya kiungo mshambuliaji, Saido Ntibazonkiza na mwajiri wake Simba SC kuna kipengele ambacho alikubaliana na viongozi kuwa ni lazima acheze kikosi cha kwanza. Tofauti na hapo labda awe majeruhi au anatumikia adhabu ndo hatopangwa kikosini," kimesema chanzo hicho.

Saido ambaye ni raia wa Burundi, aliitumikia Yanga kwa msimu mmoja na nusu kabla ya kwenda Geita ambako alicheza nusu msimu kisha kujiunga na Simba SC. Kabla ya hapo, Saido amewahi kuzitumikia timu kadhaa za Ulaya zikiwemo za Uingereza, Ufaransa na Hispania.

Je, unafikiri ni sahihi kwa timu kuweka kipengele kama hiki katika mikataba yao?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live