Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mkataba wa Moloko 'soon' unaisha

Moloko Er Mkataba wa Moloko 'soon' unaisha

Fri, 28 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mazungumzo baina ya Uongozi wa Klabu ya Yanga na wakala wa Jesus Ducapel Moloko yanatarajiwa kuanza rasmi mwezi ujao. Yanga wanataka kumbakisha winga wao Moloko kwa msimu ujao.

Mkataba wa Yanga na Jesus Ducapel Moloko unamalizika mwisho wa msimu huu wa 2022/23. Jesus Moloko amewapa nafasi kubwa Yanga kutaka kuendelea kusalia katika klabu hiyo.

Yanga walimsajili Jesus Ducapel Moloko kutokea AS Vita Club, Julai 2021, licha ya kutokuwa na msimu mzuri mwaka jana, Moloko amekuwa kwenye kiwango bora msimu huu akiisaidia timu yake kwenye michezo ya Ligi na michuano ya CAF.

Hadi sasa Uongozi wa Yanga umeshakamilisha kuwaongezea mikataba baadhi ya wachezaji wao Kama.

Wachezaji ambao tayari wameshaongezewa mikataba Yanga ni; Dickson Job, Djigui Diarra, Djuma Shabani, Yannick Litimbo Bangala, Farid Mussa, Mudathir Yahya Abbas, Bakari Nondo Mwamnyeto, Kibwana Shomari, Khaldi Aucho, Fiston Kalala Mayele.

Ibrahimu Bacca na Jesus Ducapel wapo kwenye mazungumzo ya kuongezewa mikataba mipya iliyoboreshwa zaidi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: