Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mkataba wa Mbappe kufuru PSG

Kylian Mbappe 1 1536x864 Kylian Mbappe

Thu, 3 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Tetesi zinasema, Meneja wa Real Madrid Muitaliano Carlo Ancelotti, 62, ameibuka kuwa mgombea anayewania kuwa meneja mpya ajaye wa Manchester United.

Kiungo wa Colombia aliyewahi kuichezea, Everton James Rodriguez, 30, ameiweka mguu sawa “the Toffees” baada ya kugusia uwezekano wa kurejea kwenye klabu hiyo akitokea Qatar.

Paris Saint-Germain wanajiandaa kumpa mkataba mpya mshambuliaji wake Kylian Mbappe,23 wenye thamani ya £799,000 kwa wiki ili kusalia klabuni hapo, huku Real Madrid wakimuwania pia mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa.

Tetesi zinasema, Bayern Munich, Tottenham na Arsenal zinamuwania mlinzi wa kulia wa Middlesbrough muingereza Djed Spence, 21, ambaye kwa sasa anacheza kwa mkopo Nottingham Forest.

Barcelona wana matumaini ya kumshawishi mlinzi wa Chelsea na Denmark Andreas Christensen, 25, na mchezaji mwenzake Cesar Azpilicueta, 32 raia wa Hispania kujiunga na klabu hiyo kwa uhamisho huru mwishoni mwa msimu.

Meneja wa Nottingham Forest Steve Cooper anasema kiungo mshambuliaji wa Wales, Brennan Johnson, 20, atavurugwa na mazungumzo ya mkataba mpya au nia za kutakwa na vilabu vya ligi kuu England.

Tetesi zinasema, Nyota wa UFC kutoka Ireland Conor McGregor, 33, ameonyesha nia yake ya kutaka kuinunua Chelsea baada ya mmiliki wake Roman Abramovich kusema ana mpango wa kuiuza klabu hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live