Mkataba wa miaka mitano aliosaini mshambuliaji kinda wa Kitanzania Muhsin Malima akijiunga na Zed FC ya Misri akitokea Dodoma Jiji, umemuibua msomi wa kueleza vile ulivyo na maana kwa mchezaji huyo.
Arafat Hussein ambaye ni msomi wa Kitanzania nchini humo anayetafuta shahada ya kwanza katika Sayansi ya Michezo, alisema mkataba huo mrefu wa Malima ni ishara tosha kuwa kinda huyo yupo kwenye mipango ya muda mrefu.
Msomi huyo, alisema Malima ameonakana kuwa ana kitu cha ziada kwani wapo wachezaji wengi kwenye klabu hiyo lakini ni wachache wenye mikataba mirefu.
Zed, zamani ikijulikana kama FC Masr, ni klabu ya soka yenye makao yake huko Giza, Misri. Klabu hiyo kwa sasa inashiriki Ligi Kuu nchini humo.