Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mkata Umeme Simba kukiwasha kesho

Mkata Pic Data Mkata Umeme Simba kukiwasha kesho

Wed, 16 Dec 2020 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

DIRISHA dogo la usajili limeanza rasmi leo Desemba 15, lakini Simba imethibitisha kwamba kila kitu cha kiungo wao mpya, Taddeo Lwanga kiko freshi.

Kwa mujibu wa taratibu za usajili kama mchezaji akiwa huru dirisha likishafunguka na vielelezo vyote vikiwepo, ndani ya masaa machache mchezaji anakuwa halali kuichezea klabu husika. Hiyo ikimaanisha kwamba kwenye mechi ya Simba na KMC kesho Jumatano Lwanga maarufu kama Mkata Umeme atakuwa freshi na wana imani watamuonjesha dakika kadhaa.

Simba ilimsajili mchezaji huyo akiwa huru baada ya kuachana na Tanta ya Misri ambayo hakuichezea mechi hata moja wakaamua kuachana kishikaji kila mmoja aangalie ustaarabu wake.

Mratibu wa Simba, Abasi Selemani alisema kwa upande wao wamekamilisha taratibu zote kama kuomba vibali vya kazi na makazi, ITC ya mchezaji huyo na imeshafika.

Walichofanya ni kuwakabidhi wahusika ambao ni Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF) ili kuvifanyia kazi na kutoa ruhusa kwa Lwanga kuanza kutumika ambapo kama mambo yakienda freshi mechi ijayo na KMC pamoja na ile ya Platnum atakuwa uwanjani.

“Mambo mengine kama klabu ambayo yapo kwa upande wetu tumeyakamilisha ila tunasubiri dirisha lifunguliwe na taratibu nyingine zifuate ili tupate ruhusa ya kumtumia mchezaji wetu,” alisema Selemani.

Chanzo: mwanaspoti.co.tz