Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mjukuu wa Lumumba anavyotamba kwenye ardhi ya Mwl .Nyerere

Maxi Mpiah Nzengeli Ms Mjukuu wa Lumumba anavyotamba kwenye ardhi ya Mwl .Nyerere

Mon, 30 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ukiongea kuhusu jezi namba 7 basi mawazo yako yote ni lazima yawe kwa Cristiano Ronaldo kwa sababu ameacha alama kubwa sana kupitia jezi namba 7.

Cristiano Ronaldo anasema pindi mtu anapovaa jezi namba 7, ina maana ya kwamba anabeba majukumu ya timu nzima na heshima, yani macho yote ya jukwaa huwa yanapenda kuangalia nini mtu mwenye namba 7 anafanya na Ronaldo anapenda kuhitimisha ya kwamba kuvaa namba 7 kwenye mpira ni bahati .

Baada ya mchezo kati ya Young Dar Africans dhidi ya Singida Fountain Gate niliiona hii picha huko Instagram picha, ina maudhui mengi.

Cha kwanza kabisa ni jezi ya Mwananchi , ikiwa imevaliwa na mjukuu wa Patrice Lumumba halafu namba ya bahati ya Cristiano Ronaldo imewekwa jina la Nzengeli.

Kule DRC wanamuita Kylian Mbape wao na ukifatilia hadithi ya Mbappe ni shabiki mkubwa wa Cristiano Ronaldo hapo kwenye muunganiko hawa watu watatu wanavaa jezi ya majukumu mazito kwa pamoja ubora.

Kipindi Ronaldo anaibeba Al Nassr na kipindi Kylian Mbape anaibeba PSG basi kuna mpiga picha katuonesha Tanzania kuna mtu anabeba majukumu ya namba 7 na kuibeba Yanga mgongoni mwake.

Kazi anayoifanya Mbappe wa Congo DR pale mitaa ya Jangwani na Twiga imetukuka, ndani ya dakika 7 anafunga mabao mawili na kuamua mechi.

Katika mechi 7 alizocheza, amefunga mabao 5 na kutoa assist 2, kwa kifupi amehusika katika mabao 7 ya Yanga kati ya 18 ambayo wamefunga kwenye Ligi Kuu ya NBC msimu huu.

msimu huu Tuzo ya Ufungaji Bora, Mchezaji Bora itakuwa pasua kichwa. Basi nawaambieni jijazeni sana kwa Mkapa, nendeni kwa wingi sana maana huenda mkamuona Maxi mara moja tu, na akaenda Ughaibuni.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: