Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mjipange huko! Napenda soka la kushambulia - Robertinho

ROBERTINHO KESHO.jpeg Mjipange huko! Napenda soka la kushambulia - Robertinho

Tue, 1 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Simba SC, Roberto Oliviera amesema anainjoi kuona wachezaji wake wanashambulia kwani ndiyo falsafa yake na falsafa ya Simba.

Robertinho amesema, hapendi kupaki basi halafu atambe kuwa muhimu pointi tatu, anapenda wachezaji wake wacheze kwenye eneo la mwisho la mpinzani wao ili waweze kupata matokeo.

"Narudia hata wapinzani wangu wakisikia hakuna shida, mimi napenda soka la kushambulia," alisema Robertinho akiwa kambini nchini Uturuki.

Simba wanatarajia kurejea nchini kesho alfajiri kwa ajili ya kuuanza msimu mpya wa 2023-24 wa Ligi Kuu ya NBC.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live