Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mjadala waibuka idadi makocha wa kigeni Ligi Kuu

TFF Shirikisho la mpira nchini TFF, wako tayari kupokea mapendekezo

Wed, 10 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kwa miaka ya hivi karibuni kumekuwa na ongezeko kubwa la makocha wa kigeni kuja na kufundisha katika Vilabu vya Ligi Kuu Tanzania Bara.

Hii inaweza kuwa inatoa taswira kama ishara ya ukuaji wa soka letu kama nchi hivyo kuvutia mpaka makocha wa kigeni kufanya kazi katika nchi yetu.

Lakini pia huenda uchumi wa Vilabu vyetu umeimarika kwa kuwa kuwa na Mwalimu wa kigeni gharama zake sio rahisi hata kidogo, kuanzia mshahara, makazi na huduma nyingine nyingi ikiwemo vibali vya kumruhusu kufanya kazi.

Sasa baadhi ya wadau wa soka kama wanatilia shaka utiririkaji wa Walimu wa kigeni pasipo idadi ama kiwango maalum kinachopangwa na Shirikisho la Soka nchini TFF.

Na pia kuona kama ongezeko hilo linaenda kuwanyima fursa walimu wazawa, sasa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi, Almasi Kasongo amesema;

"Kazi yetu sisi ni kusimamia chochote ambacho kinalenga kuboresha na kuinua mpira wa nchi hii kama hilo wanaona ni ajenda kwao walete hoja hiyo mezani "

"Sisi hatuna maamuzi wao wanatakiwa wakutane vilabu vyote 16, wakubaliane halafu walete shauri lao na litazungumzika na linalohitajika pia litapatikana" amesisitiza Kasongo

Sio kitu rahisi kwa Vilabu vyote kukubaliana, kwa kuwa Vilabu vyenye nguvu kubwa ya kifedha hivi sasa vinafikia mpaka hatua ya kutoka nje ya Bara la Afrika na kuajiri walimu kutoka Ulaya.

Lengo kubwa kuhakikisha wanakua na ubora wanaouhitaji ambao sio rahisi kuona ukifikiwa na Walimu wazawa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live