Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mjadala mzito sakata Simba, Yanga wizarani

Sakata Pic Data Mjadala mzito sakata Simba, Yanga wizarani

Mon, 10 May 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Wakati Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiitaka Wizara ya Michezo ipewe muda ili kutoa taarifa juu ya sakata la kuahirishwa kwa mchezo wa watani, Simba na Yanga, wizara hiyo imesisitiza kwamba inaendelea na vikao na vitakapokwisha, taarifa rasmi itatolewa juu ya sakata hilo.

Mechi ya watani hao wa jadi iliyokuwa ichezwe kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam iliahirishwa baada ya Yanga kuondoa timu uwanjani ikipinga mabadiliko ya muda wa mchezo huo uliosogezwa kutoka saa 11 jioni hadi saa 1 usiku.

Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo, Yusuph Singo ameiambia Mwananchi Digital kuwa, Serikali inaendelea na kikao kujadili juu ya tukio hilo.

"Vikao mbalimbali vinaendelea kwa mujibu wa taratibu husika vitakapokamilika taarifa zitatolewa na vyombo husika," amesema Singo.

Wakati vikao hivyo vikiendelea, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ametaka Wizara ya michezo ipewe muda ili kutoa taarifa ya tukio wakishirikiana na Shirikisho la soka Tanzania (TFF).

"Kero iliyotokea katika mechi ya Simba na Yanga iliyowakera wanamichezo hasa wapenzi wa soka na kusababisha manung'uniko, mijadala na kutojua hatma ya waliolipa viingilio vyao, tumeiagiza wizara kutoa taarifa ya mchezo wenyewe utachezwa lini?.

"Hatma ya waliolipa viingilio vyao, hivyo niwasihii Watanzania hasa waliojiandaa kuuona, kuusikia, tuipe muda wizara ya michezo itoe taarifa  wakishirikiana na TFF.

Awali rais wa TFF, Wallace Karia alisema kila aliyelipia kiingilio katika mchezo huo atarejeshewa.

"Pesa za kila mmoja ziko salama, zimeifadhiwa, hivyo hakuna atakayedhulumiwa," amesema Karia.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz