Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Miwani ya Klopp itafukuliwa 2070

Klopp Miwani Miwani ya Klopp itafukuliwa 2070

Sat, 27 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

NOVEMBA 2020. Liverpool ilifukia kiboksi kilichokua na mawani ya Kocha Jurgen Klopp, viatu vya Virgil, armband ya nahodha, Jordan Henderson.

Pia majina ya wachezaji na technical staff waliowezesha kutwaa ubingwa wa Ligi baada ya miaka 30.

Liverpool ilifanya tukio hilo kama ishara ya kuwaenzi mashujaa hao chini ya Klopp na kwamba mashabiki wetu wa miaka 50 ijayo waweze kuona historia na utamaduni wetu.

Tukio la kufukia boksi hilo lilifanyika wakati tulipokua tunahama kutoka center yetu ya zamani ya Melwood na kuhamia Axa Training Center.

Ni kama jambo hili la kuhifadhi mawani ya Jurgen lilitokea for purposely kwani mwaka mmoja baadaye yaani Agosti 2021, Klopp aliacha kuvaa mawani baada ya kufanyiwa surgery ya macho yake.

Wakati huu ambao Liverpool tuna ‘msiba’ wa Jurgen Klopp kutangaza kuwa ataondoka mwishoni mwa msimu haya ndio maandishi pekee ambayo nimeweza kuyaandika.

Atleast miaka 50 ijayo tutaziona tena mawani za Klopp.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live